Mkasa wa bosi MP3 download. Boss ze comedy video MP4 & 3gp hd download, mkasa wa bosi update 2022 download
Tulifikishwa mahakamani na kuanza kusomewa mashitaka mmoja baada ya mwingine kila mtu na kesi yake na namna ambavyo aliwasilisha ushahidi. Pia utetezi wa mtu ulihusika. Nikiwa nimekaa mahakamani katika kugeukageuka nikamwona mke wa marehemu boss wangu akiwa ndani ya mahakama. Sikujua kafikaje lakini siku hizi usafiri ni mwingi kwa Mbeya-Dar. Nadhani alikuja kwa ndege swali ni je! nani alimpa taarifa za kukamatwa kwangu? Sikujali hilo kwani akili yangu yote ilikua imezama kufikiria hukumu yangu.
Japo nilikua nahukumiwa kwa makosa ambayo sikuyatenda. Nilikaa pale kwa mda mara kuna kikatatasi nikaletewa pale. Baada ya kukifungua na kukisoma nilishtuka sana. Kilikua kimetoka kwa mke wa boss nacho kilisema.
Nilikuwa nawaza juu ya ile karatasi. Nikajisemea moyoni je! ikiwa ile mimba ni ya kwangu mama akijua itakuwaje? Na mbona toka tulipoambiwa hospitali Happy hana mimba sikuwahi kukutana naye tena. Je! happy mimba kaipata wapi? Niligeuka kumwangalia mke wa boss nikamwona akibubujikwa na machozi. Hali ile ilinifanya na mimi nishikwe na uchungu mwingi moyoni mwangu na kujikuta namwaga chozi hadharani. Hakika niliumia sana.
Basi akasema “kwa mujibu wa sheria ya jamhuri ya nchi umekutwa na hatia hivyo unahukumiwa miaka 15 jela. Na viboko 12 siku ya leo unapoingia na 12 siku ya kutoka”.
Wakati natoka mahakamani nikienda kupanda karandinga mke wa boss wangu ambae kwa wakati ule alikua kama mke wangu halali. Alianguka na kuzimia. Sikua hata na jinsi ya kumbembeleza. Wakati nimepanda karandinga kuna kitu nilikiona sikuamini macho yangu.
Niliishia kuwatamani ndugu zangu nisiweze hata kuwaaga kwa kuwakumbatia. Wakati gari inawashwa niliona yule mama mke wa boss amezinduka na anatoka nje cha ajabu alisimama kama aliyeduwaa kisha akawa anatembea kwa kasi kuelekea alipo dada na baba yangu. Alipofika akaanza kuonekana akimshangaa sana baba yangu. Alionekana kana kwamba ni mtu asiyeamini kitu fulani. Ghafla nilimsikia mzee wangu akifoka kwa sauti kuu “we mama vipi umenifananisha….?” Gari yetu ikawa taratibu inaondoka hivyo kilichoendelea pale sikujua.
Maswali yakazidi kuongezeka ina maana Mke wa boss anamfahamu baba yangu? Je! kama anamfahamu inamaana sisi hatujuani? Mbona mzee alionekana kasimama na dada lakini yule mama hakuonekana kushughulika na dada inamaana watoto wake hakuwa anatufahamu? Na je! amemfahamia wapi baba yangu?
Hakika nilijiuliza sana lakini sikua na majibu, sikuwa na jibu hata moja. Pengine majibu yangu yangepatikana baada ya miaka 15 baada ya kutoka Keko. Niliumia sana uchingu ulitawala moyoni mwangu. Mwisho tukafika Gerezani. Nilipokelewa vibaya kwa fimbo 12 siyo kama zile za shule zile za jela ni fimbo haswa… Nilikabidhiwa sare zangu na kuingia ndani.
Niliendelea kuteseka mule bila msaada wowote hakika nilikoma. Jela ilikua ni mahali pachungu kwangu. Nilikumbuka starehe zile niikua napata kwa boss za kuliliwa na wanawake nikajilaumu sana. Kisha nikaapa kuwa lazima Jane nitamwua kwa mikono yangu miwili ili nirudi tena Jela.
Nilishtuka polisi wakija na kusema huyu ndo anapiga kelele humu ndani. Basi nikiwa sijapona vidonda nikaanza kupigwa tena. Nilipigwa ambapo nakumbuka kuna afande mmoja akasema. Jamani huenda huyu mtu ana matitizo ya akili. Haiwezekani kila siku anafanya mpya. Wenzie wakasema huenda kweli tufanyaje sasa? Yule afande akasema tumpeleke hospitali akaangaliwe asije akaja kutuua wote akatumaliza bure mi nina mke atii. Alisikika afande akiwatania wenzie.